Kilimo cha nanasi kinapendelea hali ya hewa ya joto na husitawi vema katika mwinuko kati ya mita 0-1750 kutoka usawa wa bahari. Mwinuko wa mita 1300 hadi 1750 hufaa zaidi kwa uzalishaji wa nanasi kwaajili ya kusindika na mwinuko chini ya hapo hufaa zaidi kwaajili ya ulaji wa moja kwa moja. Mahitaji ya joto ni kati ya nyuzi joto 18°C hadi 35°C.
Utangulizi
Nanasi ni tunda la kitropiki, linapendwa na walaji wengi kwa sababu ya
ladha yake tamu na harufu yake nzuri. Tunda hili laweza liwa mara tu
baada ya kuvunwa, baada ya kulipika, au kama juisi. Nanasi ni chanzo
kizuri cha vitamin A na B, pia inakiwango kingi tu cha vitamin C pamoja
na madini kama vile: patasiam, magnesiam, kalsiam, na madini chuma.
Asili ya nanasi inaaminika kuwa ni Brazil na Paraguay huko Amerika ya
Kusini. Hapa Tanzania, nanasi hulimwa zaidi maeneo ya Bagamoyo, Kibaha
(Pwani), Tanga, Mtwara, Lindi, Geita na Mwanza. Lakini pia maeneo yote
ya pwani ya Tanzania yanafaa kwa kilimo cha nanasi.
Hali ya hewa inayofaa kwa ukuaji wa nanasi
Kilimo cha nanasi kinapendelea hali ya hewa ya joto na husitawi vema
katika mwinuko kati ya mita 0-1750 kutoka usawa wa bahari. Mwinuko wa
mita 1300 hadi 1750 hufaa zaidi kwa uzalishaji wa nanasi kwaajili ya
kusindika na mwinuko chini ya hapo hufaa zaidi kwaajili ya ulaji wa moja
kwa moja. Mahitaji ya joto ni kati ya nyuzi joto 18°C hadi 35°C.
Udongo unaofaa kwa kilimo cha nanasi
Kwa kilimo cha nanasi chachu (pH) ya udongo inayofaa ni 5.5 hadi 6.0, na
hustawi vizuri zaidi katika udongo tifutifu na udongo wenye kichanga
usiotuamisha maji. Ingawa nanasi huweza kustawi katika udongo wa aina
yoyote ile, udongo wa mfinyanzi haufai kwa kilimo cha nanasi.
Maandalizi ya shamba
Lima shamba kwa trekta, kwa ng’ombe ama kwa jembe la mkono kwa kina cha
sentimita 30 hadi 45. Shamba la nanasi unaweza kulilima kwa sesa
(flat-bed) au kwa matuta (furrows).
Kwa sesa: chimba mashimo kwa nafasi ya sm.60 kati ya mistari, sm.
30 kati ya miche na sm. 80 kati ya kila mistari miwili. Weka mbolea
kianzio katika kila shimo na upande, hakikisha shamba lina unyevu wa
kutosha kabla ya kupanda. Weka tani 10 hadi 15 za mbolea ya kuku, weka
pia viganja 2 vya mbolea ya zizi katika kila shimo.
Upandaji wa mananasi
Zipo aina mbali mbali za ‘mbegu’ (machipukizi/maotea) lakini yale
yanayochipua kutoka ardhini hufaa zaidi na hukomaa mapema. Chagua
machipukizi mazuri yenye umri mdogo na yenye kulingana kwa ukubwa. Iweke
miche kwenye kivuli kwa siku 3 kabla ya kuipandikiza iweze kutoa mizizi
haraka. Pandikiza mwanzoni mwa mvua za masika. Nafasi iwe sm.60 kati ya
mistari, sm. 30 kati ya miche na sm. 80 kati ya mistari miwili.
Pandikiza miche 50,000 katika hekta moja. Chovya miche kwenye dawa ya
Diazinon au Fention kwa muda wa dakika 25 kabla ya kuipandikiza ili
kuzuia mashambulizi ya wadudu.
Palizi
Palilia shamba mara kwa mara ili kuhakikisha shamba halina magugu.
Katika kilimo cha nanasi magugu hudhibitiwa kwa palizi ya jembe, kung’oa
kwa mkono ama matumizi ya viuagugu. Matumizi ya viuagugu hurahisisha
zaidi palizi ya nanasi ukizingatia kuwa nanasi huwa na miiba katika ncha
za majani yake ambazo huchubua ngozi endapo palizi za jembe zitatumika.
Njia nyingine ni matumizi ya matandazo (mulch) ya majani au plastiki
(plastic mulch) maalum kuzuia magugu.
Shamba la mananasi |
Mahitaji ya mbolea ya mananasi
Weka mbolea ya NPK gramu 50 hadi 70 kwa kila mche wakati wa kupanda.
Weka tena gramu 85 kwa kila mche baada ya miezi 3 na pia miezi 3 baadae.
Wadudu na Magonjwa yanayosumbua minanasi
Nanasi ni zao lisilosumbuliwa na wadudu ama magonjwa mara nyingi. Hii ni
faida kubwa sna kwa wakulima wa nanasi! Hivyo endapo patatokea
mashambulizi ya wadudu na magonjwa, ushauri zaidi wa kitaalam utafutwe
kukabiliana na tatizo husika. Hakikisha unakagua shamba ili kuzuia
wadudu kama wataonekana.
Uvunaji wa mananasi
Nanasi huanza kutoa maua miezi 12 hadi 15 baada ya kupanda kutegemeana
na aina ya nanasi au maotea ya mbegu yaliyotumika, muda wa kupanda na
joto la mahali husika. Kwa kawaida nanasi hukomaa miezi 5 baada ya kutoa
maua, hivyo nanasi huchukua miezi 18 hadi 24 kukomaa/kuiva. Katika
kilimo cha nanasi, mimea ikitoa maua kwa nyakati tofauti tofauti
itasababisha kuvuna kidogo kidogo na kwa muda mrefu. Kwa sababu hiyo
ndio maana ni muhimu kupanda kwa wakati mmoja mbegu zenye umri na ukubwa
sawa.
Kwa wanaofanya kilimo cha nanasi kibiashara (commercial pinapples
production) hutumia kemikali aina ya Ethrel (@ 100 ppm) mwezi mmoja
kabla ya kuanza kutoa maua ili mimea mingi iweze kutoa maua kwa wakaii
mmoja, angalau 80% ya mimea yote.
Vuna wakati kikonyo cha nanasi kimebadilika rangi kuwa njano ya dhahabu.
Kata kikonyo cha nanasi chenye urefu wa sm. 30 kikiwa kimeshikana na
nanasi na upunguzie majani ya kichungi chake.
Utunzaji wa mananasi
Hifadhi nanasi katika eneo lenye ubaridi huku kikonyo chake kikielekea
juu. Hakikisha unauza nanasi mara tu au siku 2 hadi 3 baada ya kuvuna
ili kutunza ubora wake.
Mananasi yaliyovunwa |
0 Comments