MBOLEA ZA ASILI NA VIWANDANI ZA KUPANDIA NA KUKUZIA MAZAO
Mbolea au virutubisho ni viinilishe ambavyo huitajika katika ukuaji wa mimea.Virutubisho hivi ndivyo huongeza au kufanya rutuba ya udongo.Katika mahitaji ya virutubisho ambavyo mimea huitaji vimegawanyika katika makundi mawili makuu.
1>>Virutubisho vikuu-Ambavyo ni Nitrojeni,Fosfeti, na potashi.
2>>>Virutubisho vya ziada (madini muhimu)-Ambayo ni Boroni,Salfa,Magneziamu,Molebdenamu,Zinki n.k
AINA ZA MBOLEA
Kuna aina kuu za mbolea ambazo hutumika katika kilimo na wakulima ambazo ni;
i>>MBOLEA ZA ASILI (ORGANIC FERLTILIZER)
Hizi hutoa virutubisho ambavyo ni vya asili kutokana na viumbe hai kama wanyama au masalia ya mimea yenyewe.Masalia ya mimea au kinyesi cha wanyama huongeza rutuba katika udongo.Mbolea hizi ni kama vile
a>>MBOLEA VUNDE (COMPOSITE)-Hii hutengenezwa kwa kwa kukusanya mchanganyiko wa masalia ya mimea ,samadi na majivu.Unaweza ukachimba shimo na kuweka mchanganyiko wako uvunde au unaweza ukachanganya mchanganyiko wako katika vyombo kama mapipa au mifuko migumu.
b>>>MBOLEA ZA MIKUNDE (GREEN MANURE)-Hizi hutokana na kupanda mimea jamii ya mikunde,ambayo huoteshwa na shambani na kulimwa kuichanganya na udongo iri kuongeza rutuba katika udongo.
kinyesi cha wanyama mbalimbali wanaofugwa c>>>>SAMADI (MANURE)-Hii hutokana na kama vile kuku,mbuzi,ng'ombe,nguruwe n.k
d>>>>>MAJIVU-Ni mbolea ya asili ambayo hubeba madini ya fosfeti,kalsiamu,magnesiamu na potashi kwa kiasi kikubwa.
ii>>>MBOLEA ZA VIWANDANI/KEMIKALI (INORGANIC FERTILIZERS)
Hizi ni mbolea ambazo zinatengenezwa viwandani kwa kuchanganya virutubisho mbalimbali kwa uwiano na viwango maalum vilivyowekwa ili kukidhi mahitaji ya zao husika.Tofauti na mbolea za asili mbolea hizi hutengenezwa kwa lengo la kupandia au kukuzia hivyo hulenga mahitaji halisi ya mimea.
AINA ZA MBOLEA ZA VIWANDANI/KEMIKALI
1>>MBOLEA ZA KUPANDIA
Hizi zinapaswa kutumiwa na mkulima wakati wa kupanda mazao shambani.lengo la mbolea hizi ni kusaidia kuharakisha uotaji wa mizizi na kuimarisha mizizi ya mimea katika udongo.Mbolea hizi zina virutubisho vya Fosfeti na potashi kwa kiasi kikubwa.Pia zina virutubisho kama vile nitrojeni,Boroni,Shaba,Zinki n.k
Mbolea za kupandia ni kama vile;
--Minjingu Mazao
--Minjingu Rock phosphate (MRP)
--Di Ammonium Phosphate (DAP)
--Double Super Phosphate (DSP)
--Single Super Phosphate (SSP)
--Triple Super phosphate (TSP)
--Murate of Potash (MOP)
--Nitrogen,Phosphate na Potassium (NPK)
2>>>MBOLEA ZA KUKUZIA
Mbolea za kukuzia huwekwa katika shamba baada ya mimea kuota kwa kwa lengo la kuharakisha ukuaji wa mimea hususani sehemu za majani.Kirutubisho kikukuu katika mbolea hizi ni Nitrojeni na sehemu inayobaki ni virutubisho vidogovidogo na kibeba mbolea.
Mbolea za kukuzia ni kama vile;
--UREA
--Calcium Ammonium Nitrogen (CAN)
--Sulphate of Ammonia (SA)
--NPK
FAIDA ZA KUTUMIA MBOLEA
---Kupata au kuongeza wingi wa mavuno shambani
---Kuongeza ubora wa mazao na hivyo kuweka ushindani mzuri katika soko huria.
---Mbolea huwerzesha kuhifadhi ubora na rutuba ya udongo hivyo kupunguza kasi ya uchakavu wa udongo.
---Upunguza uharibifu wa mazingira kwa kutofyeka misitu kwa ajili ya kuanzisha mashamba mapya msimu hadi msimu.
---Kupunguza gharama za kilimo kwa kutolima eneo kubwa na kupunguza au kuokoa nguvukazi ambayo ingetumika katika eneo kubwa.
1 Comments
Vipi kuhusu mbolea za kuzalishia
ReplyDelete